Google Adsense, Kujiingizia Kipato - Sehemu ya 1


Blogging imeanza kuwa kimbilio ya vijana wengi wa kizazi kipya baada ya kugundua Fursa hii ambapo kuna uwezekano mkubwa wa Mtu kujiendeshea Maisha kwa kupitia Hili. Miaka ya nyuma hili halikufikirika kwa Tanzania yetu, ila kwa nchi za wenzetu hasa Ulaya na Africa Magharibi waliliona hili Kitambo.

Miongoni mwa sababu kubwa inayowapelea Watu waanzishe Blogs ni Kujitangaza, Umaarufu zaidi au Kubwa zaidi ni KUPATA PESA. Hapa ndipo Mkazo wangu wa Leo Unaanzia. Kupitia Blogging yako una nafasi ya kujiingizia kipato kizuri tu (Vigezo na Masharti Vikizingatiwa).

Ingawa ukiwa Online na ukaandika aidha kupitia Google kwamba "Making Online" zinaweza kuja address kibao zenye ofa nzuri za kutamanisha lakini nyingi miongoni mwa hizo ni za Uongo, zitakupotezea muda na pengine kukuchukulia hela zako tu. Japo zipo Nyingi, leo naomba nikuambie kuhusiana na Hii Google Adsense, Ambayo kwa Bloggers Wengi ni Mkombozi wa Kweli.

Ni Nini hasa Hii Google Adsense?    

Ni Programu inayoendeshwa na Google ambayo humwezesha Mwandishi aliyethibitishwa ambaye yupo katika Network maalum ya Google kuweka Matangazo ambayo hujibadili Automatic Kulingana na Mazingira husika,  Matangazo hayo huwa ni katika Mfumo wa Maandishi, Picha, Video au interactive media advertisements ambazo hulenga Makundi Maalum ya Watembeleaji/Hadhira.

Adsense Ina Changamoto nyingi kwa kipindi cha zama hizi ingawa Zipo mbinu zinazoruhisiwa na namna ya kufanya ili Site yako iwe salama na kuingiza Kipato Kizuri zaidi.

Mpaka Hap kuna Swali Kuhusiana na Huu Utambulisho?....Karibu sana.


Tupate Facebook

Pata Blog Fasta

Wasiliana Nasi Tukuwezeshe Kupata Blog nzuri na yenye Viwango Vya Ubora Unaoendana na Mazingira ya Sasa. Tupigie Simu au Tuma Email:- 0719 447 204, 0752 981 380 au tzbloggers@gmail.com

Contact Form

Name

Email *

Message *

2016 © Tanzania Bloggers