Habari za Leo?
Katika Muendelezo wetu wa Kutoa Mafunzo ya Blogging hasa kwa kutumia lugha ya kiswahili, leo naomba nikufahamishe njia rahisi zaidi ya kuweka Facebook like box katika blog yako.
FUATA NJIA HIZI RAHISI
Ingia kwenye Dashboard ya Blog yako kisha Bonyeza LAYOUT
Ukishaingia kwenye LAYOUT utabonyeza Add Gadget katika Upande unaotaka Ikae Hiyo Facebook Like Page Yako Mfano Pembeni Juu Kulia.
Kisha Utabonyeza HTML/ Java Script na Kuingiza Codes hizi za HTML.
<iframe src="//www.facebook.com/plugins/likebox.php?href=http://www.facebook.com/BongoGossip&width=270&height=220&colorscheme=light&show_faces=true&border_color&stream=false&header=false&" style="border:none; overflow:hidden; width:270px; height:220px;" ></iframe>
Kumbuka kubadili Jina la BongoGossip na kuweka jina la Page yake ya Facebook, Pia una nafasi ya kubadili Urefu na upana Kutoka 220 hadi 300. Save na re load blog yako kuona mabadiliko hayo.
Karibu kwa Maswali, Maoni au Ushauri. Kila la Kheri.